
Kampuni ya TotalEnergies imewahamisha takriban wafanyakazi 1,300 kutoka maeneo mbalimbali ya Mashariki ya Kati kufuatia mashambulizi yaliyoanzishwa na Israel na Marekani dhidi ya Iran.
Huku mashambulizi ya Israel na Marekani dhidi ya Iran yakiendelea, makampuni ya kimataifa yanawaondoa wafanyakazi wao kutoka nchi za eneo hilo.
Kampuni kubwa ya nishati ya Ufaransa ya TotalEnergies imewahamisha takriban wafanyakazi 1,300 kutoka maeneo mbalimbali ya Mashariki ya Kati kufuatia mashambulizi yaliyoanzishwa na Israel na Marekani dhidi ya Iran.
Meneja Mkuu wa TotalEnergies, Patrick Pouyanne alisema wafanyakazi husika waliondolewa katika Umoja wa Falme za Kiarabu (UAE), Qatar, Saudi Arabia na Iraq. Pouyanne alisema ni idadi ndogo tu ya wafanyikazi wa ndani na wakandarasi waliobaki katika eneo hilo kudumisha shughuli muhimu.